Msamiati
Posta;sanduku la posta (SLP) Post office;post office box(P.O.Box)
barua;kuandika barua, Letter;to write a letter
barua ya ndege;kwa ndege , airmail;by airmail
Kupata barua, to get a letter
Kutuma barua , to send a letter
Kuandikiana barua, to correspond /write each other
Kujibu barua , to answer a letter
stempu;kuweka stempu; stamp(s)to put a stamp
tarishi,ma-,. Messenger(s)
Kuchukua ,kupeleka, to take,to send
ngamia ;farasi,. Camel;horses(s)
treni,basi,kwa miguu, train,bus,on foot
Sijali alikwenda posta kupeleka barua kwa rafiki yake wambura .Sijali anaishi Tanzania na wambura anaishi Kenya.Sijali na Wambura huandikiana barua mara nyingi.Kila mwaka Sijali na Wambura hukutana mara Moja Arusha au Nairobi.Mwaka Jana wambura alikuja Arusha,mwaka huu Sijali atakwenda Nairobi .Kabla ya kwenda ni lazima Sijali atangulize barua kumuelezea wambura siku na saa ya kufika.
Juzi Sijali aliipata barua kutoka Nairobi kwa wambura .Bila kukawia Sijali alijibu mara Moja,alisema;
“Mpenzi wambura ,salamu sana,Asante kwa barua Yako nzuri,nimefurahi kuisikia
Umefika salama .pole kwa safari ndefu.wewe unabahati unasafiri kwa ndege,Mimi
bado sijapanda ndege,Kila mara nasafiri kwa ndege au kwa treni,Nikipata fedha mwaka
Huu nitakuja Nairobi kwa ndege,nitakutaarifu mapema uje kunipokea uwanjani…”
Watu wengi huandikiana barua ,Barua zinachukuliwa kwa ndege,kwa treni,kwa basi na hata kwa miguu,zamani sana huko Uingerexa matarishi walikuwa wakipanda farasi kusambaza barua ,huko uarabuni wakipanda ngamia,na hapa kwetu walikwenda kwa miguu
We will continue next week