KISWAHILI FOR BEGINNERS: SIASA YA TANZANIA

We will continue with our topic SIASA YA TANZANIA

Tanzania ni nchi kubwa iliyotokana na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ,Iko Afrika Mashariki,Zamani sana waajemi,waarabu,Wahindi na baadaye wazungu walifika pwani ya Tanganyika kufanya biashara.Waarabu walikamata watumwa ,walifanya biashara ya watumwa .wazungu walileta ukoloni na ubeberu Tanganyika .

Watanzania walipigania uhuru wao,Leo Tanzania ni nchi huru,Viongozi wanasema Kila mara “Uhuru na kazi”.Kila mtu ni lazima afanye kazi.Siasa ya ujamaa na  kujitegemea ni siasa ya kazi.Lazima watanzania wote wafanye kazi kwa bidii Ili wapate kujenga nchi yao.Tanzania ina watoto wengi na wazee wachache.Watoto ni mara mbili ya wazee.Ni lazima watoto wote Hawa waende shule kupata elimu.shule nyingi zimejengwa na wananchi.Chama Cha mapinduzi (C.C.M).ndicho chama kinachotawala Tanzania .kinaamini kuwa watu wote ni sawa na kinafuata siasa ya usawa wa watu wote,bila kujali tofauti ya rangi,dini,n.k.

Watanzania wote wanajua kiswahili,lugha ya taifa lao,watanzania ni wakarimu,na ukifika utafurahi kukaa nao.Ili upate kufurahia safari Yako Tanzania,jifunze kiswahili,wageni wengi wanaokuja Tanzania wanajifunza kiswahili ;wengi wao wanasema kiswahili ni lugha rahisi kuliko lugha nyingi duniani.Anza Leo kujifunza kiswahili kwa bidii .ukitaka kujua kiswahili safi Njoo Tanzania,Baada ya kumaliza kitabu hiki.ukifika jaribu kuongea kiswahili Kila siku bila kuogopa kufanya makosa .

Zoezi

1.Tanzania Iko wapi?

2.watanganyika walipigania nini?

3.Waalabu walikuja pwani ya Tanganyika kufanya nini?

4.je Tanzania Ina watu wangapi?

5.Nani alinenga shule nyingi Tanzania

Msamiati wa kisiasa

Bunge,mbunge,uchaguzi.                                                                Parliament ;member of Parliament;election to choose

Kuchagua,                                                                                        to choose

Kugombea kura,.                                                                             to campaign for votes

Upinzani,mpinzani ,.                                                                         Opposition,opponent

We will continue with our topic next period

 

Related Articles

Back to top button