KISWAHILI FOR BEGINNERS: SHULE YETU 2

We proceed with our topic shule yetu
Kuna walimu wengi pia ,wa kike na kiume ,walimu wanaume ni mara tatu ya walimu wanawake .Dada yangu ni mwalimu katika Shula yetu .mwaka Jana alikuwa mwalimu mkuu.mwaka huu amekataa kua mwalimu mkuu,amesema ni kazi kubwa mno,hapati nafasi ya kuwatunza watoto wake nyumbani .watu wengi wanafikiri inafaa wanaume tu wawe walimu wakuu kwa sababu Wana nafasi zaidi kuliko wanawake ,hasa wanawake wenye watoto wadogo ,mwalimu mkuu wa shule yetu ni hodari sana ,watoto wote na walimu wanampenda .siku moja,aliwaambia watoto wote walete mawe ya kujenga darasa la saba.watoto walileta mawe mengi.Mwalimu mkuu pia alileta mawe Kila siku asubuhi.watoto waliweka mawe Yao pamoja.Baadaye walisimama mstarini,mwalimu mkuu akawakagua kuona kama nywele ,mikono ,miguu na nguo zao ni safi.wale ambao walikuwa wachafu wakaadhibiwa .Watoto wachache wanakwenda shule ya sekondari Kila mwaka kutoka shule yetu.tuna watoto watatu tu wanasoma chuo kikuu Cha Dar es salaam .Walimu wetu wanafanya bidii katika kazi Yao ngumu ya kuwafundiaha watoto wetu maarifa mbalimbali.
Mbele ya shule Kuna shamba kubwa ambalo hulimwa na walimu na wanafunzi .Kila mwaka wanapanda mbegu mbalimbali na wanapata mavuno mazuri .Shule yetu Haina shida ya fedha ya kununulia vifaa vya shule .Sisi wazazi pia tunasaidia katika kazi ya shamba la shule ,Kuna ushirikiano mzuri kati ya shule na Kijiji.
End of our story we will continue with new topic next time