KISWAHILI FOR BEGINNERS: PILI AKIWA SERENGETI 2

We will continue with our topic Pili akiwa SERENGETI

Tanzania Kuna mbuga kubwa ya wanyama pori .Je unajua jua jina la mbuga hiyo ?Inaitwa Serengeti,Iko karibu na mji wa Arusha. Serengeti Kuna wanyama wa Kila aina ,wakubwa na wadogo,kwa mfano : tembo,twiga,kifaru ,Simba ,chui,nyati,mbuni,swala,na wengine wengi.

Ukitaka kuwaona wanyama wote Hawa nenda Serengeti .Kila mwaka watu wengi huja Serengeti kuona wanyama, Wanatoka nchi mbalimbali :Ulaya,Marekani,Asia,na nchi nyingine.

Pili na watoto wake walisikia habari za Serengeti, Siku Moja,walikwenda kuona wanyama Serengeti ,Walipofika Arusha,walikutana na watalii wengi,wakaenda Serengeti pamoja .Pili alifurahi sana kupata nafasi hii kuwaonyesha watoto wake mbuga hii kubwa ya wanyama,japo walikuwa ndani ya gari ,Sijali aliogopa sana alipoona Simba amelala na twiga wakila majani ,Mama yake alimwambia ,”usiogope,hakuna hatari”,Mashaka na Chausiku waliongea peke Yao,sijui waliongea nini.nafikiri waliongea juu ya wanyama wa porini.Hii Ilikuwa mara Yao ya kwanza kuona wanyama wengi namna hii.

Walifurahi sana,Jioni,Pili na watoto wake walirudi Arusha mjini,wakala wa shangazi Yao,watoto wake walieleza mambo waliyoyaona Serengeti,Shangazi Yao alifurahi kuisikia hadithi zao,mwishowe alisema,”Mimi pia nitakwenda Serengeti mwaka ujao mtakapo kwenda,au mnasemaje?”Watoto walijibu wote pamoja ,”ndiyo ,shangazi,twende pamoja ;Serengeti ni kuzuri sana.

Ni Moja ya maajabu ya dunia ,au sivyo mama ?”Mama Yao alikuwa bafuni ;Hakusikia walichosema watoto wake ,kama angesikia ,bila shaka angekubaliana na watoto wake

We will continue with our topic next period

Related Articles

Back to top button