loader
Sh Bilioni 1.7  zapunguza kero vyumba vya madarasa Segerea

Sh Bilioni 1.7 zapunguza kero vyumba vya madarasa Segerea

KIASI cha Shilingi bilioni 1.7 kilichotolewa kukabiliana na athari za Covid-19 kimetumika katika ujenzi wa vyumba 86 kati ya 125 vinavyohitajika katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam. 

Mbunge wa Jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam, Bonnah Kamoli alisema hayo baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 81 vya madarasa katika shule 11 za sekondari jimboni humo, miradi inayotekelezwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia hapa nchini.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, Segera inakabiliwa na upungufu wa vyumba 39 tu vya madarasa kutoka 125 vilivyokuwa vinahitajika.

“Hili ni jambo kubwa sana na ndiyo maana tumeamua kuwaita ili tuweze kumshukuru Rais wetu kwa upendo mkubwa aliotuonesha wana Segerea,” alisema.

Alisema tayari watoto 6,893 wamepangiwa kuendelea na kidato cha kwanza katika shule 17 jimboni humo, lakini idadi ya wanafunzi waliopo kabla ya hao wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza mwakani, wakiondolewa wanafunzi 3,636 waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 19,967.

“Kwa hiyo tukiwaongeza hawa wapya 6893 wnakuwa jumla 26,860. Kwa kila ikama ya kukaa wanafunzi 45 hadi 50 kwa kila darasa.

Alisema kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali katika jimbo hilo pamoja na wadau wa maendeleo jimboni humo wanaendelea kumuunga mkono Rais Samia  kwa kujenga vyumba hivyo vinavyopungua ili kuondokana kabisa na upungufu wa vyumba vya madarasa jimboni humo.

Alisema baada ya ujenzi huo kukamilika katika shule hizo hawatakuwa na awamu mbili za kusoma vile vile mlundikano wa wanafunzi wengi katika darasa moja hivyo watoto watasoma kwa raha.

“Tumefanya ziara katika shule zote ambako kunajengwa vyumba hivi vya madarasa na tumejionea hali halisi ya ujenzi unavyoendelea. Hakika Rais amefanya jambo kubwa sana na hili ndilo limetufanya tusikae kimya.

“Tumeona tutoke tumshukuru lakini pia tuwaombe watanzania tuungane kwa pamoja ili tuweze kumuombea Rais wetu kwa mwenyezi Mungu ili aendelee kuwa na afya njema na mwili na roho apte kuendelea kutuletea maendeleo zaidi,”alisema.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Kisukuru, Lucy Lugome alisema ujenzi wa vyumba vitano katika Shule ya Sekondari Magoza vinavyogharimu sh milioni 100 umefikia katika hatua ya kupaua na kuahidi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija aliwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi na kuagiza wakuu wa shule kujipanga kwa ajili ya madawati.

Cleric held in Shinyanga over alleged sodomy 

Police in Shinyanga Region have arrested Macedonia ...

foto
Author: LUCY NGOWI

Post your comments

Advertisement

CRDB

Recent Posts

Categories

more headlines in our related posts

latest # news